2013-07-10 12:00:59

Mheshimiwa Padre Nkea Fuanya ateuliwa kuwa Askofu Mwandamizi wa Jimbo Katoliki Mamfe, Cameroon


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Nkea Fuanya kutoka Jimbo Katoliki la Buèa, kuwa Askofu Mwandamizi wa Jimbo Katoliki la Mamfe, Cameroon. Hadi kuteuliwa kwake alikuwa ni Katibu mkuu wa Chuo Kikuu Cha Kikatoliki nchini Cameroon.

Askofu mteule alizaliwa tarehe 29 Agosti 1965 ambalo kwa wakati huo lilikuwa ni Jimbo kuu la Bamenda. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa Daraja Takatifu la Upadre kunako tarehe 22 Aprili 1992 kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Buèa, Cameroon. Tangu wakati huo amefanya kazi mbali mbali za kichungaji hadi kunako mwaka 1999 hadi mwaka 2003 alipokwenda Roma kwa ajili ya masomo ya juu na kujipatia shahada ya uzamivu kutoka katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana.

Kunako mwaka 2003 hadi mwaka 2007 alikuwa ni Katibu mkuu wa Jimbo. Mwaka 2007 hadi mwaka 2010, akapelekwa kufundisha na kuwa mlezi, Seminari kuu ya Mtakatifu Thomas D'Aquin iliyoko Bamenda. Kuanzia mwaka 2010 alibahatika kupangia shughuli mbali mbali katika Baraza la Maaskofu Katoliki Cameroon, Jimbo kuu Bamenda katika masuala ya Sheria za Kanisa na hatimaye, akawa ni Katibu mkuu wa Chuo Kikuu cha KIkatoliki cha Cameroon.







All the contents on this site are copyrighted ©.