2013-07-09 12:22:47

Wamissionari wa Damu Azizi ya Yesu waanza mkutano wao mkuu wa XX mjini Roma, uchaguzi mkuu ni hapo tarehe 15 Julai 2013


Mkutano mkuu wa XX wa Shirika la Wamissionari wa Damu Azizi ya Yesu,( C.PP.S), umefunguliwa rasmi Jumatatu tarehe 8 Julai 2013 kwa Ibada ya Misa Takatifu na unatarajiwa kufungwa hapo tarehe 19 Julai, 2013. Mkutano huu unaongozwa na kauli mbiu "Jumuiya ya Kinabii inayopania kuleta mabadiliko katika Kanisa na Upatanisho Ulimwenguni".

Tangu kufunguliwa kwa mkutano huu, wajumbe wanaendelea kujadiliana mambo msingi yanayopaswa kuongoza ndoto yao kwa siku za usoni; vigezo, sifa na karama wanazozipatia kipaumbele kwa viongozi watakaochaguliwa kuliongoza Shirika katika mchakato wa kufikia malengo na ndoto ya maisha yao kama Wamissionari wa Damu Azizi ya Yesu. Uchaguzi wa mkuu wa Shirika unatarajiwa kufanyika hapo tarehe 15 Julai 2013 na baadaye kusimikwa rasmi.

Tarehe 16 Julai 2013, wajumbe watafanya uchaguzi wa washauri wakuu wa Shirika na kuanzia tarehe 17 hadi tarehe 18 kutakuwa na mkutano wa viongozi wakuu wa Shirika.







All the contents on this site are copyrighted ©.