2013-07-09 12:08:05

Mheshimiwa Padre Eduard Daher ateuliwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Tripoli, Libya


Baba Mtakatifu Francisko ameridhia uchaguzi wa Sinodi ya Maaskofu wa Kanisa la Kigiriki la Kimelkiti uliomteua Mheshimiwa Padre Archimandrita Eduard Daher, B. C. kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Tripoli, Libya. Kabla ya uteuzi huo, alikuwa ni Paroko wa St. Elie in Zahlè.

Askofu mkuu mteule alizaliwa tarehe 23 Aprili 1973 nchini Lebanon. Baada ya masomo na majiundo yake ya kitawa, akaweka nadhiri za daima tarehe 28 Agosti 1994. Akajiendeleza kwa masomo ya juu na hatimaye, kunako tarehe 8 Mei 1999 akapewa Daraja takatifu la Upadre.







All the contents on this site are copyrighted ©.