Waraka wa kwanza wa Papa Francisko:Mwanga wa Imani
Waraka wa kwanza wa Kichungaji wa Papa Francisko wenye jina: Mwanga wa Imani, "Lumen
Fidei" ulitolewa Ijumaa katika mkutano wa waandishi wa habari. Waraka huo unakamilisha
mafundisho ya kipapa juu fadhila za Kimungu; yaani: Imani, Matumaini na Mapendo,
yaliyoanzishwa na Papa mstaafu Benedikto XVI, kwa kutoa nyaraka mbili juu ya Mungu
ni Upendo "Deus Caritas Est" mwaka 2005 na Tumaini Linalookoa "SPE Salvi" mwaka 2007.
Papa
Fransisiko awali, akitangaza juu ya waraka wake wa kwanza wa kichungaji , Mwanga wa
Imani alileleza kwamba , waraka huo ni kazi ya iliyoanzishwa na Mtangulizi wake Papa
mstaafu Benedikto XVI, ambaye aliipitisha rasimu yake kwa ajili ya Papa mpya kuikamilisha.
Na kwamba ni wazi waraka huo , umeendeleza mandhari nyingi zilizo mpendeza Papa mstaafu
Benedikto XVI ikisaidiwa na msaada kutoka hati ingine ya imani na hoja, hadi katika
furaha binafsi ya kukutana na Kristu. Na katika maadhimisho ya Mwaka wa Imani miaka
50 ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican , waraka unalenga kuhamasisha mwamko mpya wa
kiini cha wajibu wa imani katika moyo wa mahusiano yote ya binadamu.
Waraka
mpya uliotolewa umetengwa katika sura nne, zinazotanguliwa na utangulizi mfupi.
Waraka huo unalenga kuonyesha jinsi imani katika Yesu Mfufuka inavyoweza kumwongoza
Muumini kuona zaidi ya mipaka ya upeo finyu unaomfungia mtu binafsi, nje ya jamii
zima katika umoja wa upendo wa Mungu. Dhana ya upofu wa imani, wenye kuzuia maendeleo
ya kisayansi na kumfanya mtu kubaki katika gizani, na kinyume chake muumini huigundua
sauti inayomwita kuuona mwanga unaoweza kuwaongoza watu wote kutoka giza la ubinafsi
kuelekea ukweli zaidi na dunia ya udugu , iliyosimikwa katika ahadi za Mungu Muumba.
Sura ya kwanza inampeleka msomaji, katika Agano la Kale na Agano jipya , tangu
wakati wa Abrahamu , aliyeisikia sauti ya Mungu ikimwita hadi wakti Waisrael wakisafiri
kuelekea mwanga wa Nchi ya Ahadi , hadi kwa kifo cha Yesu Msalabani, Kipeo cha Upendo
wa Mungu kwa binadamu. Katika sura hii ujumbe wa Papa, unatazamisha katika kuguswa
na nguvu ya upendo katika kufanya mageuzi. ikilenga kutupa mwanga zaidi katika kuelewa
mahusiano yetu na ndugu zetu katika Kristu, wake kwa waume.
Sura Pili, inasisitiza
juu ya kiungo muhimu kati ya Imani na Ukweli, ambavyo bila hivyo imani inaonekana
kuwa si kitu zaidi ya hadhithi za kufikirika na furaha za mpito zisizo weza kutudumisha
wakati wa majaribu magumu. Katika jamii ya sasa , Waraka mpya unasema , kuna mwelekeo
wa kuyaona maendeleo ya teknolojia na furaha ya mtu binafsi, kuwa ndiyo ukweli msingi,
katika mtazamo mpana juu ya masuala ya uwepo wa asili yetu kama mashaka makubwa. Bila
ya upendo katika mioyo yetu , ukweli huwa baridi, na huonekana kama kitu binafsi
na ukandamizaji usioweza kuyabadilisha maisha ya watu wengine. Lakini kwa kusikiliza
, kuona na kuamini uwepo wa Kristu katika maisha yetu ya kila siku, tunaweza kupanua
mipaka yetu ya kuona mbali zaidi na hivyo kuwa na njia zilizo bora zaidi katika kutmikia
kwa ajili ya mazuri ya wote. Mwanga wa Imani Yetu katika Kristu , unaweza kutoa mchango
mkubwa katika ufanikishaji wa matunda ya majadiliano na wasiokuwa Wakristu na wasioamini
Mungu, ukionyesha jisi wale wanaomtafuta Mungu au kuutafut ukweli wanavyokaribinswa
na kumulikiwa na Mwanga huo.
Sura ya Tatu , imesimikwa juu ya Kanisa kama
mahali ambapo mwanga wa imani unalindwa na kuenezwa kiazazi hadi kizazi. Kupitia Sakramenti
ya Ubatizo na Ekaristi, kupitia kukiri Imani, sala kwa Baba Yetu na kutii amri za
Mungu, Kanis ahufundisha lugha ya imani na kutuleta sisi katika upendo wa Utaatu Mtakasifu
ili kwamba kila anayeamini si mpweke. Na sura ya nne na ya mwisho, inalenga katika
Imani na mazuri kwa wote, na kuonyesha jinsi mwanga wa imani unavyoweza kukuza amani
na maridhiano , na kufundisha heshima katika uumbaji wa Mungu. Waraka pia unazingatia
maeneo yanayomulikiwa na mwanga huo, tangu familia iliyosimikwa katika msingi ya ndoa
na maelewano kama muungano thabtiti kati ya mwanaume na mwanamke. Imani anaandika
Papa, haiwezi kufuta mateso duniani , lakini hutusindikiza katika kukabiliana nayo
na pia hutupatia tumaini jipya katika upendo wa Mungu. Waraka huo unakamilika na Sala
kwa Bikira Maria, Mama wa Yesu, mfano wa Imani, mwenye kutuongoza sisi katika kuuona
Mwanga wa upendo wa Mungu.