Papa aweka tick azimio la kutajwa Watakatifu Yohane XXIII na Yohane Paulo II
Papa Fransisko ameweka sahihi hati yenye azimio la kutaka kuwatangaza kuwa Watakatifu,
MwenyeHeri Yohane XXIII na Mwenye Heri Yohane Paulo II. Padre Federico Lombardi,
Msemaji wa Vatican, ijumaa, alitangaza hilo kwa wanahabari mjini , baada ya kutolewa
kwa Waraka wa kwanza wa Papa Francisko, juu ya Mwanga wa Imani. Padre Federico
Lombardi alitangaza baada ya Papa Francisko , kukutana na Kardinali Angelo Amato,
Mkuu wa Shirika kwa ajili ya Utajaji Wenye Heri na Watakatifu, ambamo Papa alipitisha
azimio hilona kuitisha kikao maalum cha Baraza la Makadinali( Consistory) kujadili
kwa kina hoja ya kumtangaza kuwa Mtakatifu , Papa Yohane Paulo 11. Na pia alipitisha
pendekezo la kuwa na kikao cha kawaida cha Decania ya Makardinali na Maaskofu juu
ya kumpandisha katika ngazi ya Utakatifu , Mwenye Heri Yohane XX111. Akieleza
tukio hilo linalo onekana kidogo kama si la kawaida, Padre Lombardi aliwaambia wanahabari
kwamba, licha ya kukosekana kwa muuzija wa pili, ni mapenzi ya Papa Francisko kwamba,
Utakatifu wa Papa Mkuu wa wakati wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, Yohane XXIII,
unatambuliwa rasmi wakati huu maadhiinisho ya miaka 50 ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa
Vatican. Padre Lombadi pia alieleza kwamba, bado utajaji Utakatifu , unathaminiwa
hata bila ya muujiza wa pili kutokea , katika maana kwamba, tayari kuna muujiza wa
kwanza ulioongoza Yohane XX111, kutajwa Mwenye Heri. Na pia alitaja uwepo wa majadiliano
ya wanateolojia na watalaam,yanayotazama ulazima wa kuwa na miujiza miwili kwa ajili
ya mtumishi wa Mungu kutajwa Mwenye Heri au Mtakatifu. Ni wazi, Padre Lombardi aliongeza,
Papa anayo mamlaka yote juu ya muujiza wa pili. Pamoja na hayo, mpaka sasa hakuna
tarehe iliyotajwa kwa ajili ya matukio hayo, iwe kikao cha Cosistory au lini watatangazwa
kuwa Watakatifu. Padre Lombardi ameonyesha tumaini lake kwamba bila shaka itakuwa
kabla ya mwisho wa mwaka.