2013-07-06 15:35:31

Mwakilishi wa Vatican alilia maadili katika matumiziya teknolojia.


Askofu Mkuu Silvano Tomasi, Mtazamani wa Kudumu wa Jimbo Takatifu katika Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa, yenye Makao yake makuu mjini Geneva, Alhamis, akitoa maoni yake katika kikao cha ngazi ya juu cha Baraza la Uchumi, alionyesha kufurahia mchango chanya unaofanikishwa na huduma za kisayansi na teknolojia katika maendeleo ya binadamu. Lakini pia alisisitiza haja ya uwajibikaji wa kimaadili katika matumizi ya teknolojia.

Askofu Mkuu Tomas ameitaka jumuiya ya kimataifa, wakati huu inapotafuta mbinu mpya za kupambana na umaskini na uboreshaji wa ubora wa maisha kwa ufanisi zaidi, kwamba ,kikao hicho cha ECOSOC , kina wajibika pia kujali uadilifu katika sayansi na teknolojia, vumbuzi na uwezo msingi wa utamaduni, kwa ajili ya kukuza maendeleo endelevu, katika utendaji wote wa taratibu za mageuzi katika njia mpya zinazo gunduliwa.
Na alionyesha kukubaliana kwamba, mafanikio ya jumla ya sayansi ya maendeleo ya binadamu, teknolojia na uvumbuzi (STI) ni muhimu katika kusaidia maeneo mengi katika dunia inayobadilika, kuchukua nafasi ya mazingira mapya ya kimataifa. Alieleza na kutaja mifano michache kama gunduzi za dawa mpya, kwa mfano, zile za kurefusha maisha kwa watu waliapatwa na athari ya kinga ya mwili kuathiriwa na virus vya ukimwi. Hata hivyo akaonya dhidi maendeleo yenye kutafuta tu faida za kiuchumi au teknolojia,kwamba peke yake hayatoshi, kwa kuwa maendeleo ya kweli yanahitaji ya juu ya yote, kuwa ni kweli na muhimu, kama vile kuzingatia matarajio ya kila binadamu, kubaki kuwa jambo msingi na changamoto isiyoweza kuepukwa.
Na hivyo, heshima ya utu wa binadamu inakuwa ni kipimo msingi katika mwendelezo wa maarifa na maendeleo yote ya kiSayansi,ki teknolojia na ugunduzi mpya. Wakati huo huo, kuchukua dhamana ya kijamii katika kuonyesha mshikamano na nchi maskini,hasa katika maisha ya msingi ya mahusiano ya binadamu, katika taratibu za sayansi na teknolojia. Umuhimu wa utamaduni wa ukweli, unabaki kuwa kigezo muhimu katika mantiki zote za uwezo wa akili ya binadamu na katika elimu yote ya kuuelewa ulimwengu na mambao yanayomzunguka.
Mbali na hilo, maarifa ni matokeo ya kazi ya uchambuzi, uchunguzi na tafakari zilizofanyika tangu zama za kale , kuwa urithi wa kawaida wa binadamu. Ndiyo maana ya haki miliki hulinda uvumbuzi huo kwa muda ulio kubalika na baada ya hapo inakuwa ni suala la umma na kwa huduma ya watu wote.

Askofu Mkuu Tomas Silvano alitaja mambo mawili msingi kwamba, kwanza ni haja ya uwajibikaji wa kimaadili katika matumizi ya sayansi na teknolojia. Pili, katika kuwa na mshikamano wa kweli thabiti katika uendelezaji wa elimu ya kisayansi na uhamishaji wa teknolojia, kwamba vinafanyika katika misingi ya uadilifu wa kimaadili kwa manufaa ya binadamu wote.

Askofu Mkuu alieleza kwa kujali kwamba, mara nyingi maendeleo ya watu, yamechukuliwa katika mtazamo wa aidha kukuza uchumi, kukomboa bei katika masoko, kuondolewa kwa ushuru,kukuza uwekezaji katika uzalishaji, na Mageuzi ya kitaasisi - kwa maneno mengine, kama tu suala la ujanja wa kiufundilenye kujali faida binafsi. Lakini pamoja na haya yote kuwa ni muhimu, tunapaswa kujiuliza , kwa nini basi ufundi huu daima umekuwa na matokeo ya kutoridhisha. Tunahitaji kufikiri kwa bidii sababu zake. .Askofu Mkuu alitaja kwamba, kamwe uhakika wa maendelea ya kudumu hauwezi kufanikishwa kikamilifu kwa nguvu za mtu mmoja mmoja , iwe katika soko au katika juhudi za siasa za kimataifa. "Maendeleo hayawezekani bila kuhusisha watu wema na wanawake, bila wafadhili na wanasiasa wenye dhamiri njema, wanaotafuta mema kwa ajili ya watu wote.







All the contents on this site are copyrighted ©.