2013-07-05 08:44:05

Mahujaji kutoka Tanzania wanatembelea Roma, Lourdes na Nchi Takatifu


Katika Maadhimisho ya Mwaka wa Imani, waamini wanaalikwa kwa namna ya pekee kufanya hija ya maisha ya kiroho kama sehemu ya mchakato wa kujipatia neema na baraka zinazotolewa na Mama Kanisa. RealAudioMP3

Padre Raymond Saba, katibu mkuu, Idara ya Uchungaji, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania katika mahojiano maalum na Radio Vatican anasema kwamba, kuna mahujaji 41 kutoka Tanzania wanaotembelea: Roma, Italia; Lourdes, Ufaransa na Nchi Takatifu.

Kundi hili la mahujaji kutoka Tanzania linafanya hija mjini Roma kwa kuwa hapa ni Makao Makuu ya Kanisa Katoliki, mahali ambapo kuna makubiri ya miamba wa imani, Mitume Petro na Paulo, walioyamimina maisha yao kwa ajili ya Kristo na Kanisa lake, changamoto na mwaliko wa kuifahamu, kuiungama, kuiadhimisha, kuiishi na kuisali imani hii. Watanzania hao wanatembelea Lourdes, Ufaransa kwani hii ni sehemu muhimu sana katika kukuza na kuenea kwa Ibada ya Bikira Maria, Mama wa Mungu na Kanisa.

Padre Raymond Saba ambaye ndiye mkuu wa msafara huu kutoka Tanzania anasema, wanapenda kufanya hija Nchi Takatifu kwani hapa ni chimbuko la Imani ya Kikristo. Hii ni hija ambayo itawachukua takribani wiki mbili.







All the contents on this site are copyrighted ©.