2013-07-04 12:00:30

"Siyabonga Tata Madiba"!


Ndugu na Jamaa ya Mzee Nelson Mandela wanasema kwamba, hali ya Mzee Madiba inazidi kuwa mbaya siku hadi siku na kwa sasa anapumua kwa kusaidiwa na mashini. Wakati wowote madaktari wake wataweza kutoa taarifa rasmi kuhusu maendeleo ya Mzee Madiba ambaye kwa wiki tatu hivi mshumaa wa maisha yake unaendelea kupambana na mawimbi makali.

Wananchi wa Afrika ya Kusini na wapenda amani kutoka sehemu mbali mbali za dunia wanaendelea kuimba, kusali na kukesha kwa ajili ya Mzee Madiba, wakiyaweka maisha yake mikononi mwa Mwenyezi Mungu.







All the contents on this site are copyrighted ©.