2013-07-04 14:57:42

Papa Francesco: Mkristu ni mwana wa Mungu na hakuna anayeweza kuuiba utambulisho huo.


Baba Mtaktifu Fransisko amesema hakuna anayeweza kuwaibia wabatizwa utambulisho kuwa wana wa Mungu , utambulisho walio pokea kama zawadi toka kwa Mungu, kupitia kwa Yesu Kristu. Papa ameeleza wakati akiongoza Ibada ya Misa mapema Alhamis hii, katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta , ndani ya Vatican. Ibada aliyoiongoza akisaidiana na Kardinali Telesphore Placidus Toppo, Askofu Mkuu wa Ranchi India. .
Kiini cha ujumbe wa homilia yake , ulilala zaidi katika injili ya uponywaji wa mtu aliyepooza, Yesu, alimosema, ” Jipe moyo mwanangu umesamehewa dhambi zako “
Papa Fransisko alisema, pengine hili lilimtisha kidogo mtu huyu, kwa sababu yeye alitaka kuponywa mwili. Na katika uso wa upinzani wa walimu wa Sheria , waliona kama Yesu anakufuru kusema dhambi zako zimesamehewa, kwa sababu waliamini ni Mungu tu anayeweza kusamehe dhambi" . Lakini Yesu alimponya kwa vyote kimwili na kiroho pia.
Papa amesema katika tukio hili, tunapata kuuona utukufu wa Yesu, na nguvu ya maneno yake dhidi ya unafiki, na hivyo inakuwa ni alama ya jambo kubwa zaidi kwamba, Yesu anao uwezo wa kusamehe dhambi. Na hivyo, kupitia kwake, mtu anajipatanisha na Mungu, hili ni fumbo kubwa katika wokovu wa binadamu.

Maridhiano haya yanakuwa ni ufanywaji upya wa dunia , utume wa kina katika kazi ya ukombozi ya Yesu, zaidi ya yote ya sisi wenye dhambi. Na Yesu hafanyi utume huo kwa maneno , wala si kwa ishara, wala si kwa kutembea barabarani tu, hapana ila kwa kuutoa mwili wake . Ni yeye aliye Mungu aliyekuja na kukaa kati yetu , kwa ajili ya kutuponya kwa ndani, sisi wenye dhambi. "

Yesu alituweka sisi huru dhidi ya dhambi kwa yeye kuchukua dhambi zetu. Na hili hutufanya kuwa viumbe wapya. Uumbaji mpya uliofanikishwa kwa Yesu kuuvua utukufu wake Msalabani hadi kifo cha Msalaba ambako alipaza sauti yake , Baba, kwa nini umeniacha. Huu ni utukufu wa Mungu na sauti hiyo ndiyo iliyotupa wokovu wetu":

Papa Fransisko aliendela kusema, Hiii ni tendo kubwa alilolifanya Yesu , lililo tuwezesha kuwa wana huru wa Mungu. Yesu aanatupa uwezo wa Kumwita Mungu 'Baba'. Lakini daima hatuna ushujaa huyo wa kumwita Mungu Baba. Kumwita Mungu Baba kwa uhuru kamili . Tendo jema liinalonyesha kutambua uwepo wa Yesu aliyejishusha hadi kifo kwa ajili ya kutupatanisha na Mungu Baba , sisi watumwa wa dhambi, akituponya hadi katika kilindi moyo wetu . Anatufanya tufikiri mengi mema ya kuwa watoto wa Mungu , kwa sababu mtoto aliye nyumbani ni Yesu , anayetufungulia mlango wa nyumba nasi tunaingia humo.

Na alihitimisha kwa kurudia kueeleza nini maana ya Maneno ya Yesu aliposema, Haya, mwana, umesamehewa dhambi zako wewe."

Papa ameyataja maneno hayo kuwa ni msingi wa ushujaa wetu , katikakuwa huru na Mwana wa Mungu. Bwana wa Beema alitambua veyma utume wake , Mungu aliyejifanya kwua binadamu , Mung Mwana aliyetupa heshima pia kuiwa wana huru wa Mungu kuitia neema ya neno lake la upatanisho. Tunaokolewa kwa Yesu Kristo! Na hakuna mtu anaweza kuiba kadi hii utambulisho. Na anaitwa hivyo , Mwana wa Mungu , ni kadi yenye utambulisho mzuri wa ajabu. Ni kadi ya inayoonyesha raia huru. Na iwe hivyo. "








All the contents on this site are copyrighted ©.