Mamlaka ya Usalama wa Fedha Vatican yajiunga na Mtandao wa fedha wa Kimataifa
Mamlaka ya Usalama wa Fedha Vatican, ( Vatican Financial Intelligence Authority (AIF)
imekubaliwa kujiunga katika mtandao wa kimataifa wa wa Kikundi cha Egmont, ambacho
huunganisha Vitengo vya Usalama wa Fedha (Units Financial Intelligence (FIU)) katika
ngazi ya kimataifa.
Katika Mkutano wake Mkuu wa 21, uliofanyika Sun City
Afrika Kusini, kikundi cha Egmon, kilikubali kuuingiza AIF ya Vatikan kama mwanachama
kamili.
Wanachama wa kikundi cha Egmont, huhakikisha uwepo upatikanaji
wa misaada katika mtandao wa kimataifa wa FIUs na wenye kuwezesha kubadilishana
habari katika mapambano dhidi ya uhalifu wa kifedha. Hatua hii kwa Jimbo la Papa
na jijji la Vatican, ni alama ya hatua mbele zaidi, katika mchango wake kwenye
juhudi za kimataifa, kupambana na uhalifu wa kifedha. .
Kundi Egmont lilianzishwa mwaka
1995 na sasa wanachama ( FIUs) zaidi ya 130 za kitaifa. Ni jukwaa la FIUs duniani
kote na katika kubadilishana habari na kuratibu mapambano dhidi ya fedha haramu na
ufadhili wa ugaidi.