Jaji mkuu wa Mahakama kuu aapishwa kuwa Rais wa kipindi cha mpito Misri!
Bwana Adly Monsour, aliyekuwa Jaji mkuu wa Mahakama kuu ya Misri ameapishwa rasmi
siku ya Alhamisi kuwa Rais wa Misri katika kipindi cha mpito, hadi hapo uchaguzi mkuu
utakapofanyika tena, baada ya Jeshi kumwondoa kutoka madarakani Rais Mohammed Morsi.
Hadi sasa tarehe rasmi kwa ajili ya uchaguzi mkuu bado haijapangwa.
Jeshi
limeamua kujitwalia madaraka baada ya mamillioni ya wananchi wa Misri kuandamana kutaka
Rais Morsi kujiuzuru kutoka madarakani, lakini akagoma kutekeleza sauti ya umma!