2013-07-03 15:10:16

Papa Fransisko ajichanganya na maskini wa Roma


Zaidi ya watu 200 maskini wa Roma walihudhuria chakula cha jioni, kilichoandaliwa siku ya Jumatatu jioni katika Bustani za Vatican, karibu na Pango la Bikira Maria wa Lourdes, ambako watu wa kujitolea, waliwahudumu khafla hiyo. Ilikuwa ni Siku Kuu kubwa iliyoandaliwa na Chama cha “Circolo di San Pietro (CSP)“ kwa ajili ya watu wahitaji na kwa heshima ya Papa Fransisko, khafla iliyohudhuriwa pia na Kardinali Giuseppe Bertello, Rais wa Utawala wa Jiji la Vatican, na Rais wa Chama cha CSP mheshimiwa Leopoldo Torlonia.
Monsinyori Franco Camaldo, Mhudumu msaidizi wa kikanisa katika chama cha Circolo di san Petro, akilizungumzia tukio hili, amelitaja kwamba , ilikuwa ni wakati wa furaha kubwa, si kwa wageni wao tu lakini hata kwao kwa kupata heshima ya kuandaa mlo huo wa jioni na kwa ajili ya maskini na Papa.
Na baada ya mlo , wageni walipewa zawadi ya mifuko miwili , mmoja ukiwa wa matunda na mwingine ukiwa na keki kutoka Naples, iliyotolewa kama zawadi kwa chama chake, na pia waliwapatia zawadi ya Keyholder yenye kuwa na picha ya Papa Fransisko.
Chama hiki cha Circolo di San Pietro, historia yake ina zaidi ya miaka 144 ya historia, na daima hujishughulisha katika kazi za mshikamano na watu maskini. Na katika miaka hii migumu ya kiuchumi, ni wazi idadi ya watu wahitaji imeongezeka kwa kasi kubwa.
Mansinyo Camaldo, aliendelea kueleza kwamba, hata utambulisho wa wateja wao umebadilika utambulisho wa wateja wao, na ufafanuzi mziri zaidi juu ya chama hikini kama ilivyoelezwa na Mwenye Heri Yohane Paulo II, ni mkono wa upendo wa Mtakatifu Petro kwa maskini wa Roma. Na hiyo ndio daima, utume wake, kama ilivyojionyesha dhahiri wakati wa vita kuu yapili ya dunia, iliitwa jicho la Papa ambakowatu walikwenda kupata sopo ya Papa.
Na kwamba awali waliofika katika jiko hilo walikuwa ni wageni toka nje ya Italia lakini kwa wakati huu, pia kuna maskini wengi waitaliano wanaokwenda kuomba msaada katika chama hicho, ambao kutoka na mgogoro wa kiuchumi , wanashindwa kufika mwisho wa mwezi.
Na kwamba licha ya mahitaji ya haraka yakiwmili kama chakula na mavazi, kwa kwua hawana fedha za kununua vitu hivyo, pia wanahitaji kupata upendo na mshikamano kutoka kwa watu wengine.
Chama hiki ambacho awali kiliitwa pia “Senti ya Petro”, ambacho saasa jina linabadilika tena na kuwa Senti kwa Upendo wa Papa , kama ilivyokuwa siku zote , katika makanisa 150 wanachama, kwa muda wa siku tatu 28-30 June, hukusanya sadaka maalum, na pia kutoka katika Makanisa Makuu manne ya Kipapa ya Hapa








All the contents on this site are copyrighted ©.