2013-07-02 09:05:34

Walioathirika kwa vitendo vya kigaidi Jijini Dar es Salaam kunako mwaka 1998 wakumbukwa!


Mke wa Rais Barack Obama wa Marekani Mama Michelle na Mama Salma Kikwete wa Tanzania pamoja na watoto wao, Jumatatu, tarehe Mosi, Julai 2013 wametembelea Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam ambako kuna hifadhi ya kumbu kumbu za waathirika wa bomu lililopigwa kwenye Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania tarehe 7 Agosti 1998 na kuua zaidi ya watu 12 na wengine 85 kujeruhiwa. Katika tukio kama hilo, Jijini Nairobi, watu 44 walifariki dunia, wakiwemo raia 12 kutoka Marekani.







All the contents on this site are copyrighted ©.