2013-07-02 09:28:17

Misri kuna waka moto! Rais Obama ateta na Rais Mursi wa Misri!


Wakati hali ya kisiasa nchini Misri inaendelea kuwa tete, huku mamillioni ya wananchi yakiandamana, mawaziri wakijiuzuru na jeshi kuwa katika hali ya hatari, Rais Barack Obama wa Marekani amemsihi Rais Mohamed Mursi wa Misri kujadiliana na waandamanaji hao kama njia ya kumaliza mgogoro ambao unatishia maisha na usalama wa wananchi wengi wa Misri.

Rais Obama amezitaka pande zote kuhakikisha kwamba, maandamano yanakuwa ni salama, baada ya watu zaidi ya 16 kupoteza maisha yao kutokana na maandamano ambayo yanaendelea kutikisa viunga vya miji mbali mbali ya Misri. Serikali ya Marekani inapenda kudumisha misingi ya demokrasia nchini Misri, kumbe haiungi kikundi chochote nchini Misri kwa sasa.

Mgogoro wa kisiasa unaweza kuhitimishwa kwa njia ya mchakato wa kisiasa, kadiri ya Rais Obama, wakati akiwa Jijini Dar es Salaam.







All the contents on this site are copyrighted ©.