2013-07-02 10:04:34

Hatimaye, Obama na Bush wakutana Dar!


Rais Barack Obama wa Marekani na Rais Mstaafu George W. Bush wa Marekani kwa pamoja, Jumanne tarehe 2 Julai 2013 wameshiriki katika kumbu kumbu ya watu waliofariki dunia wakati Ubalozi wa Marekani Jijini Dar es Salaam ulipolipuliwa kwa bomu kunako mwaka 1998.

Wachunguzi wa mambo wanasema, haya ni matukio machache sana ambayo Marais hawa wawili wameonekana kwa pamoja hadharani. Wameweka shada la maua na baadaye kushikana mikono na ndugu na jamaa ya wale walioathirika kutokana na mlipuko huo. Rais mstaafu George W. Bush yuko Jijini Dar es Salaam ili kushiriki mkutano wa wanawake ulioandaliwa na Taasisi ya Bush katika mchakato wa kuwajengea uwezo wanawake Barani Afrika.







All the contents on this site are copyrighted ©.