2013-07-01 07:38:16

Zimbabwe inayo fursa na haki ya kufanya uchaguzi huru na wa haki!


Rais Barack Obama wa Marekani wakati wa ziara yake nchini Afrika ya Kusini, Jumapili tarehe 30 Juni 2013 amesema kwamba, Zimbabwe ambayo kwa sasa iko kwenye mchakato wa kukua kwa uchumi wake, inayo fursa nyeti ya kuhakikisha kwamba, uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika nchini humo kwa mwaka huu, unakuwa huru na wa haki.

Hii inatokana na ukweli kwamba, Zimbabwe kwa sasa inaongozwa na Katiba Mpya na kwamba, uchumi wake unaanza pia kukua kwa kasi nzuri, kumbe, uchaguzi huru na wa haki ni jambo linalowezekana. Rais Obama ameyasema hayo wakati akizungumza na umati wa vijana kwenye Chuo Kikuu cha Cape Twon, nchini Afrika ya Kusini. Rais Obama amesema, Zimbabwe ilipigania uhuru kwa nguvu nyingi na matokeo yake ikajikuta ikitumbukia katika uchu wa madaraka, hali ambayo imepelekea kuanguka kwa uchumi wa Zimbabwe.







All the contents on this site are copyrighted ©.