Jumatatu ya tarehe 8 Juli 2013, Papa Fransisko, atafanya ziara ya nusu siku katika
kisiwa cha Lampedusa Italy. Taarifa zinasema, ,akiwa ameguswa na taarifa ya kuzama
kwa mashua iliyokuwa imebeba wahamiaji na wakimbizi waliolenga kuingia Italy bila
kibali, hivi karibuni, wahamiaji kutoka Afrika, ikiwa moja ya matukio ya namna hiyo
mfululizo, Papa anania ya kwenda kuwaombea wale wote waliopoteza maisha yao baharini
, na pia kukutana na waathirika na wakimbizi waliopo sasa katika kisiwa hicho. Pia
anakwenda kuonyesha mshikamano wake na watu wa kisiwa hicho na kuhimiza uongozi na
wote wenye mamlaka kuwajibika zaidi, kwa ajili ya kuhakikisha kwamba, huduma nzuri
ni zinatolewa kwa watu wakimbizi na wahamiaji hao , wake kwa waume, ambao sasa wanaishi
wako katika shida na mahangaiko makubwa.