Papa Fransisko asema: sala inahitaji kuwa jasiri na kung'ang'ana
Tunapaswa kuomba kwa ujasiri kwa Bwana, na kung'ng'ania kama alivyofanya Abrahamu.
Ni himizo lililotolewa na Papa Fransisko , mapema Jumatatu hii wakati wa Ibada ya
Misa, aliyo iongoza katika Kanisa ndogo la Mtakatifu Marta, hapa Vatican. ambamo alielezea
juu ya kuomba, kwamba ni kufanya mazungumzo na Bwana, kama Yesu alivyofundisha.
Katika
Ibada hii Papa aliiongoza akisaidiana na Kardinali Kurt Koch, Rais wa Baraza la Kipapa
kwa ajili ya Kukuza Umoja wa Kikristo na Katibu wake, Askofu Brian Farrell, na ili
hudhuriwa na wajumbe na wafanyakazi wa Baraza hilo.
Papa alielekeza homilia
yake zaidi katika somo la kwanza, ambamo mna maelezo jinsi Abrahimu alivyotolea maombi
yake kwa Bwana kwa ujasiri na king'ang'anizi, ili ausalimishe mji wa Sodoma licha
ya madhambi yaliyokuwa yakifanyika katika mji huo. Papa Fransisko alionyesha kuushangalia
ujasiri huu wa Abrahim, kwa jinsi alivyopata nguvu za kuendelea kuzungumza uso kwa
uso na Bwana, akiutetea mji huo wenye madhambi mengi, kama yanavyo sema Maandiko
Matakatifu.
Papa alitafakati ujasiri huo, akianisha na wakati wetu, akisema,daima
sisi tunapozungumzia ujasiri hufikiri juu ya ujasiri wa kitume, wa kwenda nje kuhubiri
Injili na mambo kama hayo. Lakini kumbe, pia kuna aina nyingine ya ujasiri, ni ujasiri
katika kutolea maombi mbele za Bwana. Ujasiri ambao mara nyingi, waamini hawana, wengi
hukata tamaa haraka na kutokomea. Papa alieleza huku akionyesha mshangao kwa jinsi
Ibrahimu anavyoshikilia ombi lake bila kuchoka hadi Bwana akamtimizia haja yake.
Na ndivyo muumini anavyotakiwa kuomba kwa ujasiri na bila kuchoka , katika kuitetea
haki hata ya mtu mmoja, ni kuomba wokovu hata kwa ajili ya mtu mmoja. Papa aliendelea
kusema kwamba, ni lazima kuomba kwa imani neema za Mungu na kumwacha yeye atende.
Na alikumbusha kwamba, Yesu mwenyewe anatuambia kwamba lazima tuombe kama mjane
au kama yule hakimu au kama yule mtu aliyekwenda kwa jirani yake katikati ya usiku
na kubisha hodi mlangoni kuomba msaada kwa jirani yake, alibaki akigonga hadi jirani
yake alipomtimizia haja yake. Nasi waamini ndivyo tunavyotakiwa kuomba kwa imani,
tukiendelea kunga'ngana hadi hapo Bwana atakapo timiza haja zetu kwa fadhila yake
mwenyewe. Papa anasema ni vizuri kufanya hivyo. ,Maombi hayo ya Ibrahim, yanarejea
katika moyo wa Yesu na kutufundisha, ombeni kwa ujasiri : maana Baba yeny anajua mnayo
yahitaji.
Papa Fransisko alieleza na kuitazama zaidi zaburi ya 102: 'Mhimidini
Bwana, Ee nafsi yangu; na yangu yote, lisifu jina lake Takatifu... na kusema kwamba,
kwa naombi yaliyomo katika zaburi hii, tunajifunza mambo tunayopaswa kusema kwa
Bwana wakati tunaomba neema.