2013-07-01 07:52:36

Kamwe msiboreke! Wamegeeni wengine furaha inayobubujika kutoka katika undani wa mioyo yenu!


Jumapili iliyopita, tarehe 30 Juni 2013 Kanisa limeadhimisha Siku ya Ukarimu wa Khalifa wa Mtakatifu Petro, ambayo waamini wanaalikwa kwa namna ya pekee kutoa michango yao ya hali na mali kwa ajili ya kuchangia huduma ya upendo inayotolewa na Baba Mtakatifu sehemu mbali mbali za dunia.

Papa Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, jumapili iliyopita, anawashukuru waamini wote kwa sala na mshikamano!

Katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitando ya kijamii, anakumbusha kwamba, kamwe Mkristo hapaswi "kuboreka" wala kuchukia. Anayempenda Kristo ni mtu aliyesheheni furaha ambayo anawamegea wengine!







All the contents on this site are copyrighted ©.