2013-06-28 14:20:43

Padre Pierbattista Pizzaballa, O.F.M. ateuliwa na Papa kuwa Mlinzi mkuu wa Nchi Takatifu na Mlima Sion


Baba Mtakatifu Francisko ameridhia uteuzi wa Padre Pierbattista Pizzaballa, O.F.M. kuwa mlinzi mkuu wa Nchi Takatifu na Mlima wa Sion kwa kipindi cha miaka mitatu.

Kuanzia Oktoba 1990 amekuwa akitekeleza utume wake kwenye Nchi Takatifu, kama Jaalim wa Kihebrania, Mkuu wa Jumuiya ya Watakatifu Simeone na Anna iliyoko mjini Yerusalem. Amekuwa ni msaidizi wa karibu wa Patriaki wa Yerusalem katika shughuli za kichungaji, alikwisha wahi kuwa ni Makamu wa Patriaki kunako mwaka 2005 hadi mwaka 2008. Kunako mwaka 2004 aliteuliwa kuwa ni Mlinzi mkuu wa Nchi Takatifu na Mlima Sion.







All the contents on this site are copyrighted ©.