2013-06-27 09:39:37

Wasi wasi watanda Afrika ya Kusini!


Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini amefuta ziara ya kikazi nchini Msumbiji ambako alikuwa ashiriki katika mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, SADC unaojadili kuhusu miundo mbinu, ili kuwa karibu na Familia ya Mzee Nelson Mandela ambaye hali yake kwa sasa inazidi kuwa mbaya. Kwa sasa kimya kikuu kinaendelea kutawala Afrika ya Kusini kwa hofu kuhusu hatima ya Mzee Nelson Mandela aliyesimama kidete kupinga utawala wa ubaguzi wa rangi, akabahatika kuwaunganaisha wananchi wa Afrika ya Kusini. Kwa hakika Mzee Madiba ni jembe la nguvu!







All the contents on this site are copyrighted ©.