Baba Mtakatifu Francisko ameunda Tume ya Kipapa kwa ajili ya Benki ya Vatican, (IOR)
itakayofanya upembuzi yakinifu kuhusu masuala ya kisheria na shughuli mbali mbali
zinazofanywa na Benki hii ili hatimaye, kufanya maboresho mintarafu maisha na utume
wa Kanisa la kiulimwengu na Vatican katika ujumla wake. Tume hii inatekeleza katika
mapana yake mabadiliko ambayo Baba Mtakatifu anapenda kufanya katika taasisi zinazoisaida
Vatican kutekeleza utume wake.
Tume hii itakuwa na wajibu wa kukusanya taarifa
kuhusu utendaji wa shughuli za Benki hii na taarifa yake kuwasilishwa kwa Baba Mtakatifu
Francisko. Benki hii itaendelea kutekeleza wajibu wake mintarafu sheria ya mwaka 1990
iliyotolewa na Mwenyeheri Yohane Paulo wa pili au kama itakavyoamriwa vinginevyo na
Baba Mtakatifu Francisko.
Tume ya Kipapa kwa ajili ya Benki ya Vatican inaundwa
na Jopo la watu watano kama ifuatavyo:
Kardinali Raffaele Farina, Rais wa Tume. Kardinali
Jean Lous Tauran, Mwanachama. Monsinyo Juan Ignacio Arrieta Ochoa de Chinchetru,
Mratibu Monsinyo Peter Bryan Wells, Mwanachama. Professa Mary Ann Glendon, Mwanachama.