2013-06-27 09:17:18

Shirika la Wafuasi wa Kristo kufanya uchaguzi mkuu 2014


Baba Mtakatifu Francisko ameridhia dhamana ya kitume aliyokabidhiwa Kardinali Velasio De Paolis, kuwa ni mwakilishi wa kipapa kwa ajili ya Shirika la Wafuasi wa Kristo, hadi uchaguzi mkuu wa Shirika hili unaotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa Mwaka 2014.

Itakumbukwa kwamba, Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa kumi na sita, kunako mwaka 2010 alimteua Kardinali De Paolisi kuwa ni msimamizi wa kitume wa Shirika la Wafuasi wa Kristo, (Legionari di Cristo).

Baba Mtakatifu Francisko anampongeza Kardinali De Paolis kwa kazi kubwa aliyokwishaifanya hadi sasa na kwamba, amesoma kwa umakini mkubwa taarifa aliyompelekea kuhusiana na hali ya Shirika hili kati ya mwaka 2009 hadi mwaka 2010.

Uchaguzi mkuu utakuwa na dhamana ya kuwachagua viongozi wakuu wa Shirika; kupitisha muswada wa Katiba Mpya ambao Baba Mtakatifu mwenyewe ataupitia kabla ya kuanza kutumika rasmi. Lengo ni kusaidia mchakato wa mageuzi ndani ya Shirika hili.







All the contents on this site are copyrighted ©.