Maaskofu wasikitishwa na hukumu ya Mahakama kuu nchini Marekani!
Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani limesikitishwa na hukumu iliyotolewa na Mahakama
kuu ya Marekani kuhusu sheria iliyokuwa inalinda ndoa ambayo ilianza kutumika kunako
mwaka 1996 kuwa ni batili na kinyume cha Katiba. Tangu sasa watu wa jinsia moja wanaoishi
kama mme na mke watakuwa na haki sawa kama watu wengine wanaoishi katika ndoa.
Katika
taarifa iliyotiwa sahihi na Kardinali Timothy Dolan, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki
Marekani anasema, kwamba, ndoa ni taasisi ya pekee inayomuunganisha mwanaume na mwanamke
katika maisha na kwamba, watoto ni zawadi ya muungano huu wa upendo. Watoto wana haki
ya kuwa na wazazi wa pande zote mbili yaani: Baba na Mama, changamoto kwa viongozi
wa Jumuiya ya Kimataifa kulinda na kutetea maana hii ya ndoa.