2013-06-27 11:30:06

Caritas na mikakati ya msaada wa dharura kwa waathirika wa vita nchini Mali


Kamati tendaji ya Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki nchini Mali, imehitimisha kikao chake cha siku mbili, kilicho jadili pamoja na mambo mengine, utoaji wa msaada wa dharura kwa watu walioathirika kwa migogoro na vita Kaskazini mwa Mali. Wajumbe wa kamati wamezungumzia kuhusu upatikanaji wa fedha zitakazogharimia miradi mbali mbali inayoendeshwa Kaskazini mwa Mali.

Kwa pamoja, Mali imeamua kushirikiana na Mashirika mengine manne ya Caritas Ukanda wa Sahel unaojumuisha nchi za: Burkina Faso, Niger, Senegal na Mali yenyewe. Mashirika mengine ya misaada yanayochangia gharama kwa kiasikikubwa ni Caritas Italia, Caritas Hispania na Shirikisho la Misaada ya Kanisa Katoliki Kimataifa, Caritas Internationalis.

Msaada huu unawalenga hasa watu wasiokuwa na makazi maalum, wakimbizi na Jumuiya ambazo zimeathirika na vita nchini Mali. Caritas Ukanda wa Sahel itawezeshwa ili kukabiliana na changamoto hizi katika kuratibu na mambo ya mawasiliano ili Caritas iweze kutoa huduma bora zaidi kwa walengwa.







All the contents on this site are copyrighted ©.