Baraza la Kipapa la Utamaduni kwa kushirikiana na wadau mbali mbali, Jumapili tarehe
23 Juni 2013 waliaandaa Treni maalum kwa ajili ya watoto wenye umri kati ya miaka
sita hadi kumi waliosafiri kutoka Kaskazini mwa Italia hadi Roma na kupokelewa na
Baba Mtakatifu Francis aliyewashukuru kwa kufika mjini Vatican.
Baba Mtakatifu
amezungumza na watoto hao kwa njia ya maswali na majibu. Waandaaji hao wamemshukuru
Baba Mtakatifu kwa kuwaonjesha upendo na ukarimu. Watoto wamepata bahati ya kutembelea
Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.