2013-06-24 09:02:36

Tamasha la Muziki katika Maadhimisho ya Mwaka wa Imani


Baraza la Kipapa la uhamasishaji wa Uinjilshaji mpya linaloongozwa na Askofu mkuu Rino Fisichella, mwishoni mwa Juma, liliandaa tamasha la muziki kwa ajili ya Maadhimisho ya Mwaka wa Imani, lililofanyika mjini Vatican. Katika salam na matashi mema kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko, alionesha pia kusikitishwa kwake kwa kutoweza kushiriki katika tamasha hili kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake.

Baba Mtakatifu katika ujumbe wake uliosomwa kwa niaba yake na Askofu mkuu Rino Fisichella, aliwashukuru wadau mbali mbali waliowezesha kufanikisha tamasha la Muziki kama sehemu ya Maadhimisho ya Mwaka wa Imani. Ni tukio ambalo limewapatia fursa ya kusimama kidogo na kuinua mioyo yao ya furaha na tafakari ya kina. Askofu mkuu Fisichella anasema, muziki ni furaha na kiungo kwa watu mbali mbali.







All the contents on this site are copyrighted ©.