2013-06-21 10:47:46

Uchaguzi nchini Madagascar bado hali ni tete!


Uchaguzi mkuu ambao ulikuwa umepangwa kufanyika nchini Madagascar hapo tarehe 24 Julai 2013, unaonekana "kupigwa dana dana" baada ya Bi Beatrice Atallah, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kuonesha wasi wasi wake, hali ambayo imezua hasira kubwa kutoka kwa viongozi wanaogombea Urais nchini humo.

Wagombea uchaguzi wanaitaka Serikali ya mpito kuhakikisha kwamba, uchaguzi mkuu nchini Madagascar unafanyika katika tarehe iliyopangwa na kamwe hawawezi kukubali kuahirishwa kwa zoezi hili. Sheria inapaswa kuchukua mkondo wake.

Kati ya wagombea wanaotarajiwa kutoana jasho jembamba ni Rais wa Kipindi cha Mpito Bwana Andry Rajoelina, aliyeingia madarakani kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi kwa kuungwa mkono na Vikosi vya ulinzi na usalama nchini Madagascar. Wengine ni Bwana Didier Ratsiraka na Bibi Lalao Ravalomanana.







All the contents on this site are copyrighted ©.