2013-06-21 10:32:14

Uchaguzi mkuu nchini Zimbabwe umeahirishwa kwa muda wa majuma mawili!


Rais Robert Mugabe ameiomba Mahakama kuu ya Zimbabwe kuahirisha uchaguzi mkuu nchini Zimbabwe kwa kipindi cha majuma mawili zaidi, badala ya kufanyika tarehe 31 Julai 2013 kama alivyokuwa amepanga hapo awali.

Kabla ya uamuzi huu wa Rais Mugabe, upande wa upinzani ulionesha hali ya kutoridhika katika mgawanyo wa madaraka baada ya Rais Mugabe kufanya maamuzi haya makubwa bila kumshirikisha Waziri mkuu Bwana Morgan Tsvangirai, ambaye alikuwa amependekeza kwamba, uchaguzi ufanyika tarehe 25 Agosti 2013. Viongozi wa SADC pia walikwisha mshauri Rais Mugabe kuahirisha tarehe ya uchaguzi kama sehemu ya kulinda na kudumisha amani na utulivu nchini Zimbabwe.







All the contents on this site are copyrighted ©.