2013-06-21 15:17:17

Madhabahu ya Lourdes yafungwa kwa muda ...


Hali mbaya ya hewa iliyokumba eneo la Kusini Magharibi mwa Ufaransa , iliyosabisha watu wawili kupoteza maisha, pia imesababisha madhabahu maarufu ya Bikira Maria wa Lourdes ya nchini Ufaransa, kufungwa kwa muda, kutokana na tope lililoingia katika eneo hilo. Hali iliyosababisha maelfu ya mahujaji waliotoka pande mbalimbali za dunia, kuwa ni nia za hija katika madhabahu ya Uponyaji ya Massabielle, Lourdes, kushindwa kufika katika madhabahu hayo ambako Mama Bikira Maria alimtokea Mtakatifu Benardetta Soubirous mwaka 1858.
Pdre Nicola Ventriagilia , mmoja wa waratibu katika madhabahu hayo , katika mahojiano na Redio Vatican, ameeleza kwamba, kwa wakati huu, hakika maafa ni dhahiri, kama ilivyokuwa Octoba, tope na maji vilijaa hadi ndani ya pango, kwa sasa hata kanisani na makandokando yake. Hivyo uongozi umeamua kulifunga eneo hilo kwa muda.
Kwa hali hiyo, viongozi wa Madhabahu hayo, wametangaza kuahirisha shughuli zote za Ibada na hija katika madhabahu hayo, ili waweze kupashughulikia ipasavyo.

Na wanategemea kama mvua hazitendelea kunyesha, wataweza kufungua tena shughuli za madhabahu hayo wiki ijayo, lakini kwa wakati huu hakuna atakayeruhusiwa kuingia katika eneo hilo. Na wameomba mshikamano wa sala na hali , ili kurudisha madhabahu hayo katika hali yake ya kawaida. Na wanashukuru kwamba , mpaka sasa wamepokea misaanda mingi kwa ajili hiyo.
Padre Nicola , amesema wameipokea hali hiyo ya mafuriko pia kwa moyo wa shukurani kwamba, inawawezesha kuelewa na kuguswa na imani na upendo mkuu wa watu wanaokuja kuhiji katika madhabahu hayo toka pande mbalimbali za dunia. Na wameona ishara nyingi zinazo wahimiza kuongeza bidii za kusafisha eneo hilo. Waaamini wanapahitaji mahali hapo kutolea sala zao.








All the contents on this site are copyrighted ©.