Zaidi ya wakimbizi 20,000 wamekufa maji wakijaribu kuvuka Bahari ya Mediterania!
Jumuiya ya Kimataifa inaadhimisha Siku ya Wakimbizi Duniani wakati ambapo kuna maelfu
ya watu wanaendelea kupoteza maisha yao. Inakadiriwa kwamba, zaidi ya watu 20,000
wamefariki dunia wakijaribu kuvuka Bahari ya Mediterania, wakitafuta usalama na ubora
wa maisha Barani Ulaya.
Wakimbizi wanaoishi nchini Italia wanakabiliwa na hali
ngumu ya maisha, hasa wale wanaotoka katika maeneo ya vita na kinzani kama vile Syria,
Lebanon, Yordan, Afrika ya Kaskazini, Somalia na Eritrea. Idadi ya wakimbizi wanaoomba
hifadhi ya kisiasa inazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka, lakini hali bado ni mbaya
hasa katika kambi za wakimbizi. Haya yameelezwa na Mfuko wa kuhudumia Wakimbizi wa
Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, Migrantes.