2013-06-20 11:28:59

Umoja wa Mataifa walaani shambulizi lililofanywa na Kikundi cha Al Shabaab mjini Mogadisho


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki-Moon amelaani vikali shambulio lilofanywa na kikundi cha Waaasi cha Al Shabaab kwenye Makao ya Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa mjini Mogadisho, Somalia, Jumatano, tarehe 19 Juni 2013.

Katika shambulizi hili watu kadhaa walipoteza maisha yao. Wachunguzi wa mambo wanasema kwamba, Kikundi cha Shabaab bado kina nguvu ya kuendesha mashambulizi.







All the contents on this site are copyrighted ©.