2013-06-20 07:32:38

Siku ya Vijana Duniani, mwisho wa kujisajili!


Vijana wote wanaotaka kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya 28 ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2013 yanayoongozwa na kauli mbiu “basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa ni wanafunzi” yanayofanyika mjini Rio de Janeiro kuanzia tarehe 23 hadi tarehe 28 Julai kuhakikisha kwamba, wanajiandikisha haraka iwezekanvyo kwani mwisho wa kujiandikisha ni hapo tarehe 20 Juni 2013, saa 5:59 Usiku kadiri ya saa za Brazil. RealAudioMP3

Mwaliko huu pia unatolewa kwa wahusika wote kuhakikisha kwamba, wanakamilisha pia malipo yao katika siku, ili taratibu nyingine ziweze kuendelea kutekelezwa kwani hili ni tukio linalotarajiwa kuwakusanya makundi makubwa ya vijana kutoka sehemu mbali mbali za dunia.

Ni jambo la muhimu sana vijana kujisajili ili waweze kuwa ni sehemu ya wale watakaoshiriki rasmi katika Maadhimisho haya, jambo litakaloliwezesha Baraza la Maaskofu Katoliki Brazil kuweza kujipanga kuhusu: malazi, chakula na usafiri. Kimsingi ni tukio linalowashirikisha vijana na watu wote wenye mapenzi mema, lakini kutakuwepo na maeneo maalum ambayo wataingia wale tu wenye vitambulisho maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2013.

Makundi ya vijana yafanye mipango yake kwa njia ya wakuu wa makundi haya, lakini hata vijana wenye uwezo na jeuri yao wanaweza kushiriki bila wasi wasi wowote. Gharama ya kila mtu anayeomba kushiriki katika Maadhimisho haya ni kuanzia dolla za kimarekani 300 na kiwango cha chini kabisa ni dolla 250.








All the contents on this site are copyrighted ©.