2013-06-20 09:00:04

Papa asema, dharirisho la kumpenda adui, mna utajiri mkubwa wa kiroho


Ni vigumu kuwapenda maadui zetu, lakini ndivyo Mungu anavyotutaka tufanye. Papa alieleza siku ya Jumanne asubuhi wakati akiongoza Ibada ya Misa katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta mjini Vatican.
Alisema ni lazima tuombe kwa ajili ya wale wanaotuchukia na walio tukosea, ili mioyo yao ya jiwe igeuke kuwa nyama, wapate kuusikia faraja na upendo wa Mungu wenye kuangazia wote jua na kunyeshea mvua wote ,wema na wabaya, wenye haki na wasio haki,na ndivyo Mkritu anavyopaswa kufanya.

Papa Francis alianza hotuba yake na mfululizo wa maswali juu ya mafundisho haya , na hasa zaidi juu ya matendo ya huruma na ubinadamu . Na kwa jinsi gani tunaweza kuwapenda adui zetu? Kama kweli inawezekana kuwapenda hata wanaoamua kutupa mabomu na kuua watu wengi ? au wale wanaotafuta kutoa dawa za kuua wengine , au wale wanaopenda kuvuna kiurahisi mahali wasipo pahangaikia kama vile wevi na majambazi wenye silaha. .. n.k. Papa alisema kwa guvu za binadamu , inaoonekana ni vigumu kumpenda adui . Lakini hilo ndilo Yesu analowataka wafuasi wake wafanye. Yesu akiwa mlimani alitangaza mageuzi katika sheria ya Mlimani Sinai kwa sheria mpya ya mlima wa Heri. Na kwamba sisi sote tuna maadui lakini pia kwa kina sisi pia tunaweza kuwa maadui wa wengine kwa kutowatakia mema wengine.
Papa alieleza na kutahadharisha kwamba, utakatifu si tu kwa ajili ya maisha mateule kama watawa wa kujifungia ndani, bali ni haki kwa maisha yakila siku, kwa kuwa tunatakiwa kufanya kama Yesu anavyotaka tufanye kila siku, kusamehe maadui zetu na kuwaombea.
Papa katika fundisho hili aliainisha mambo mawili, kwanza ni kumkiri Baba, mwenye kuangazia nuru wazuri na wabaya, na mwenye kunyeshea mvua kwa wenye haki na wasiokuwa na haki . Hilo alisema, linaonyesha kwamba, Mungu huwapenda wote. Na kisha aliendelea. , Yesu anatuambia tuwe wakamilifu kama Baba wa Mbinguni alivyo Mkamilifu, maana yake ni kuuiga upendo mkamilifu wa Baba wa Mbinguni. Aliongeza Yesu aliwasamehe maadui zakena kufanya kila lililowezekana kuwasamehe. Hivyo kwa mtazamo huo , ulipizaji visasi kinakuwa si kitendo cha Kikristu.
Na kwa namna gani tunaweza kufanikiwa kuwapenda maadui zetu? Ni katika kuwaombea, kama Yesu alivyofundisha, salini na waombea maadui zenu, Waombeeni w ale wanaowaudhi. Sema kwa Mungu , badilisha mioyo yao migumu na uwape moyo wa laini wa nyama ya upendo, upole na wema..
Papa alikiri kwamba ,kumpenda adui , kunaweza kutufanya tuonekane maskini , kama tumedharirisha heshima ya utu wetu. Lakini, alikumbusha , katika umasikini mna mbengu ya ustawi na upendo kwa wengine. Kama umaskini wa Yesu ulivyokuwa neema ya wokovu kwa ajili yetu sote, pia kwetu ni utajiri mkubwa kwa maisha ya milele. Papa alieleza na kuitolea Ibada ya Misa hiyo, kwa ajili ya wale ambao hawana upendo kwa wengine , ambao Yesu alijitoa mhanga kwa ajili yao na kwa ajili yetu pia.
Hivyo hili linakuwa ni fundisho la hekima ambalo ni gumu lakini zuri sana, kwa sababu, linatufanya tufanane na Baba Yetu, ambaye huwaangazia jua wote wazuri na wabaya. Hutufanya kufanana zaidi na Mwana wake Yesu, aliyetahayarishwa na kuwa maskini kwa ajili ya kututajirisha sisi kupitia umaskini wake.







All the contents on this site are copyrighted ©.