Kardinali Leonardo Sandri, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya
Mashariki na Rais wa ROACO, Jumanne, katika Ukumbi wa Kanisa la Mtakatifu Maria la
Transportina, Roma, aliongoza Mkutano wa Mwaka wa Shirikisho linalounganisha misaada
Katoliki kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki (ROACO)
Hotuba ya kufungua Mkutano
huo iliyotolewa na Kardinali Sadri ililenga katika mambo manne, kwanza , ukuu wa
adhimisho la Fumbo la Ekaristi Takatifu kwamba, muumini hujikuta ndani ya moyo wa
Mungu kwa njia ya upendo wa msalaba na ufufuko wa Bwana watu Yesu Kristu , ambamo
Roho Mtakatifu hutoka bila kipimo kwa kila anayempokea. Na alitoa mwaliko kwa kila
mjumbe wa mkutano huu ,kujifunua, kuwajibika na kujidhaminisha kwa Mungu, na kuelekeza
nia nzote kwa ajili ya mazuri kwa watu wote wa Mashariki ya Kati, wakijiruhusu kuongozwa
na neema zake Mungu.
Na kwamba, kipaumbele chao kinabaki kuwa kilekile ,
mshikamano thabiti wa Kikristu, wenye kupata dhamana yake kupitia mawasiliano ya
mara kwa mara na Maaskofu na Wachungaji wa Makanisa kijimbo, ambayo hushirikiana na
vyombo vya ROACO,pamoja na shughuli za uratibu unaotolewa kwa hiari na Umoja wa ROACO,
katika kutoa jibu kwa mamlaka ya Askofu wa Roma, ambalo ni kueneza katika mipaka
yote, kwa watu wote wa Mashariki, udugu na kujali wengine.
Kardinali aliendelea
kuzama katika fumbo la Ekaristi akisema, daima huwezesha kuamusha ari mpya ya neema
inayotuwia kuwa na deni kwa Mungu, Kristo akiwa madhabahu yetu yasiyoweza kuharibiwa.
Na ni Yeye Kuhahi Mkuu wa milele. Yeye mteswa asiyekuwa na doa ambaye alifanyika
kuwa sadaka yetu wenyewe kamili , ambayo ni pamoja na zawadi ya maisha yetu kwa Mungu
katika utii wa imani.
Kwa sababu Kristo hutuunganisha naye Mungu, , na hivyo
hutuwezesha na kudumu katika safari ya kuelekea kwenye ukamilifu wa kikristo, hata
hivyo, yenye kudai, kwa kuwa ni kipimo kwa upendo kinzani wa Msalaba. wapendeni adui
zenu na kuwaombea wale wanaowadhulumu ninyi.
Kardinali pia aliwakumbuka pia
wafadhili wa Makanisa ya Mashariki, wotei walio hai na marehemu. Na pia wengi ambao
pia wanajiunga katika mateso ya Wakristu wa Mashariki kwa namna moja au nyingine,
kwao wote wanastahili shukurani na heshima kubwa kwa kuwa washariki wa kuubeba msalaba
huu wa mateso makubwa yanayoendelezwa katika nchi ulikozaliwa Ukristu.
Alitolea
sala ili Bwana, awawezeshe Wakristu Mshariki ya Kati, kupata ujasiri, upole, uvumilivu
na nguvu za kuyaishi hayo wakiwa wamejawa na faraja ya imani, pamoja na wale wanaoshiriki
katika hatima yao ya kutisha. Na ili kamwe wasishikwe na harahara za kutaka kutoa
jibu la chuki kwa chuki; au kulipa kisasi , au kushakia uwezo neema ya Mungu, katika
hatima ya kuvunja uovu mwingi.
Na mwisho aligeukia uwepo wa "Wakuu na Mababa"
ya Makanisa Kikoptic na Kikaldayo, na Wajumbe wa Kitume na Wajumbe wengine, akisema
, wote kwa pamoja wamejumuika kama kundi moja , kutolea kilio chao kwa ajili ya amani
Mashariki ya kati. Na wakiwa na lengo moja la kuwakumbatia katika Bwana, waamini
wote wa Makanisa ya Mashariki, waliomo ndani ya Mashariki ya kati na hata sehemu mbalimbali
za dunia, kama matokeo, ya hofu za kuteseka na waliopoteza makazi yao ya asili, hasa
mizizi yao ya kiroho.
Katika mtazamo huo na kwa maombezi ya Mama Maria Mtakatifu
Sana mfano wa ukarimu wa kimama , na awadumishe wote katiak moyo wa upeondo na ukarimu
usio na mashaka kwamba Bwana ndiyemwenye kumweka mtumwa huru na ndiye anayewatangulia
katiak safari yamaisha hapa duniani mwenye kumtia nguvu mjane na yatima, lakini
njia ya waovu huiangamiza. Amina