2013-06-19 07:17:20

Zawadi kwa Maadhimisho ya Mwaka wa Imani


Katika Maadhimisho ya Mwaka wa Imani, Shirika la Posta nchini Italia limetoa zawadi ya magari madogo mawili kwa Baraza la Kipapa la uhamasishaji wa Uinjilishaji Mpya, kwa ajili ya matumizi ya Maadhimisho ya Mwaka wa Imani. Haya ni magari ambayo hutumiwa na wafanyakazi wa Posta kwa ajili ya kusambaza barua nchini Italia.

Askofu mkuu Rino Fisichella, Rais wa Baraza la Kipapa la uhamasishaji wa Uinjilishaji Mpya amelishukuru Shirika la Posta Italiani kwa mchango wake katika Maadhimisho ya Mwaka wa Imani, unaotarajiwa kufungwa rasmi, Mwezi Novemba, 2013.







All the contents on this site are copyrighted ©.