2013-06-19 07:44:45

Watu wakimbia makazi yao kutokana na vurugu Sudan ya Kusini


Mapigano yaliyojitokeza hivi karibuni kati ya Jeshi la Serikali ya Sudan ya Kusini pamoja na Kikundi cha Waasi katika eneo la Jonglei, yamepelekea idadi kubwa ya watu kuyakimbia makazi yao kwa kuhofia usalama wa maisha yao. Shirika la Habari la Misna linasema kwamba, kuna watu zaidi ya elfu kumi na moja wanaotafuta msaada wa dharura kutoka Juba.

Wananchi hao wanalazimika kutembea kwa miguu umbali mrefu kabla ya kupata msaada wa dharura unaotolewa na Mashirika ya Misaada ya Kimataifa Mjini Juba.







All the contents on this site are copyrighted ©.