Viongozi wa Makanisa wapewa mafunzo ili kusimamia vyema mchakato wa uchaguzi mkuu
nchini Zimbabwe!
Zaidi ya viongozi 200 wa kidini nchini Zimbabwe wamepewa mafunzo maalum yatakayowasaidia
kufuatilia kwa ukaribu zaidi mchakato wa uchaguzi mkuu nchini Zimbabwe unaotarajiwa
kufanyika mwaka huu. Mafunzo haya yalitolewa na Taasisi ya Kiekumene ijulikanayo kama
"Christian Action Trust Zimbabwe" (CAT-Zim). Taasisi hii ina mpango wa kutoa mafunzo
kwa viongozi wa Kanisa wapatao 5,000, ili kuhakikisha kwamba, mchakato wa uchaguzi
mkuu nchini Zimbabwe unakuwa huru na wa wazi.
Kwa miaka kadhaa, Zimbabwe imekuwa
ikishuhudia machafuko na madhulumu ya kisiasa yaliyopelekea taabu na mateso ya wananchi
wa Zimbabwe ambao bado wanaendelea kulipia kasoro hizi. CAT-Zim ni mwanachama wa
Baraza la Makanisa Ulimwenguni. Tarehe ya uchaguzi bado inaendelea kusababisha malumbano
nchini Zimbabwe.