Kwa fumbo la ubatizo sote tunakuwa viungo vya mwili mmoja wa Kristu, kanisa lake...Papa
.
Katekesi ya Baba Mtakatifu Fransisko kwa mahujaji na wageni, imeelendelea kuitafakari
sala ya Imani , na leo akitazamisha zaidi katika Kanisa kama Mwili wa Kristu. alisema,
Ndugu zangu wapendwa: Katika katekesi yetu juu ya sala ya Imani, leo tunaona Kanisa
kama mwili wa Kristo. Kwa njia ya zawadi ya Roho Mtakatifu, tuliye mpokea katika Ubatizo,
kimuujiza tunaunganishwa na Bwana kama kiungo cha mwili mmoja ambao Yeye ndiye ni
kichwa. Na kwamba mfano wa mwili wa fumbo hili hutuwezesha sisi kuutambua umuhimu
wa kuimarisha umoja wetu na Kristo kwa njia ya maombi ya kila siku,kusoma neno la
Mungu, na kupokea sakramenti. Papa Fransisko alieleza na kurejea waraka wa Mtume
Paulo kwa Wakorintho, ambamo amesema kwamba, Mwili wa Kristo, ni mmoja ulioumbwa
kwa viungo vingi. Na Ndani ya usharika wa Kanisa, na katika muungano na Papa na Maaskofu,
kila mmoja wetu ana sehemu ya kutenda, na zawadi ya kushirikishana , huduma ya kutoa,
katika kuujenga Mwili wa Kristo kwa upendo. Papa aliwahimiza waamini kumwombe
Bwana, ili atusaidie sisi kukataa kila aina ya utengano na migogoro tangu katika
familia zetu, parokia na Makanisa. Na wakati huo huo, tuombe neema kufungua mioyo
yetu kwa wengine, ili kukuza umoja na kuishi kwa amani na mapatano kama viungo vya
Mwili mmoja wa Kristo, tukivuviwa na zawadi ya upendo unao miminwa na Roho Mtakatifu,
ndani ya mioyo yetu.
Baada ya katekesi Papa alisamu katika lugha mbalimbali
kulingana na lugh, pia akitaja makundi mbalimbali ya kijamii, vijana, wazee wanadoa
wapya na bila kuwasahau wagonjwa. Kwao wote aliwapa baraka zake za Kipapa.
Na
Mapema asubuhi, Papa Fransisko katika homilia yake alisema, Ukristo si kujifunza sheria
na mausia tu , kwa kuwa kufanya hivyo kunaweza kuia kuelewa na kuuishi ukweli kwamba
Mungu ni Mungu wa furaha na ukarimu. Papa alieleza wakati wa Ibada ya Misa mapema
Jumatano hii katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta ndani ya Vatican.. Aliyarejea
masomo ya siku akisema, wanafiki waandishi na mafarisayo, waliwabebesha watu wa Mungu
mizigo ya sheria wasizoweza kuzibeba wao wenyewe na hivyo kuwaelekeza watu katika
njia ya kifo. Papa alieleza kwa kutafakari tabia tofauti tofauti kati ya waandishi
na Mafarisayo, kama ilivyoandikwa katika Injili ya Mtakatifu Matayo ambamo mna wale
wanaopenda kujionyesha wakati wa kusali, kufunga na kutoa sadaka. Lakini Yesu anawaambia
wanafunzi wake mtoapo sadaka, sala na kufunga ni lazima iwe ni siri ili Baba anayeona
sirini apate kuwapa ujira wenu. Papa aliukosoa unafiki wa mafarisayo akisema si
tu yalikuwa majivuno ya Mafarisayo na wanasheria , lakini pia hata leo kuna wenye
kupenda kushinikiza sheria nyinginyingi ngumu kwa aamini. Aliwaita watuwa namna
hiyo kuwa ni manafiki , wasomi wasiokuwa na busara za kumtafuta Mungu , na kumwelezea
Mungu katika muono mpana , na hivyo wanajizuia wao wenyewe na wengine pia kuuingia
Ufalme wa Mungu.
Papa alifafanua, kumbe Bwana anazungumzia kufunga, maombi
na Zaka, kuwa mihimili mikuu mitatu ya uchaji wa Kikristo, kwa ajili ya uongofu wa
ndani, ambayo hupendekezwa na Kanisa kwetu sote hasa wakati wa kipindi cha Kwaresima.
Pia alionya hata katika njia hii, kuna wanafiki, wanaopenda kujionyesha kwa kufunga,
kutoa sadaka na kuomba. Papa ameasa , unafiki unapoingia katika hatua hii ya mahusiano
na Mungu , inakuwa ni kutenda dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu.