Waluteri na Wakatoliki- kuadhimisha pamoja siku ya Mageuzi
Kutoka Migogoro hadi Ushirika, ndivyo inavyoitwa hati ya pamoja ya Walutheri na Wakatoliki,
inayo elezea safari yao ya kiekumeni ya miaka 50 iliyopita, wakati wakitazama mbele
katika maadhimisho ya pamoja ya kutimia kwa miaka mia tano (500) ya Mageuzi katika
Kanisa hapo mwaka 2017.
Jumatatu, Hati ya pamoja ya Tume ya Kimataifa ya
Walutheri-Wakatoliki juu Umoja, iliwasilishwa katika mkutano wa waandishi wa habari,
katika makao makuu ya Kilutheri, mjini Geneva. Hati inatazama kwa kirefu zaidi,
sababu msingi za migawanyiko iliyotenganisha makanisa haya katika karne ya 16. Hivyo
Tume , inashughulikia changamoto za uponyaji kumbukumbu hizo na kufanya kazi pamoja
kwa ajili ya upatanisho na utoaji wa shuhuda kwa maoja duniani.
Mada zilizochunguzwa
katika hati ni pamoja na msingi mandhari ya teolojia ya Martin Luther kwa lengo la
mazungumzo kati ya Waluteri na Waktoliki, na pia inalenga katika kanuni tano za uekumeni
, na kwa ajili ya mahusiano kati ya Makanisa yote, wakati wa adhimisho la pamoja
kwa 2017.
Tarehe 31 Oktoba 1517, mtawa wa Ujerumani na msomi na mwana teolojia,
Martin Luther, alitundika hoja zake 95, katika mlango Kanisa la Castle Wittenberg,
alizoona zina haja ya kufanyika kwa haraka mageuzi. Mageuzi yaliyosababisha si
tu utengano kati ya Makanisa ya Kiprotestanti na Wakatoliki, lakini pia kwa kiasi
kikubwa kutoa changamoto nzito juu ya nafasi ya dini katika jamii.
Jumatatu
, Mons. Mathiya Turk , Mkuu wa Mahusiano kati ya kanisa Kiluteri na Kipapa Baraza
la Kipapa kwa ajili ya Kukuza Umoja wa Kikristo, akiwa ameongozana na Rais wa Baraza
hilo la Kipapa, Kardinali Kurt Koch, mjiini Geneva, waliwasilisha hati kwa pamoja
katika wa vyombo vya habari. Mathiya Turk, akizungumza na Phillipa Hitchen, juu
ya umuhimu wa hati hiyo ya pamoja , aliitaja kuwa ni muhimu sana kihistoria baada
ya karne nyingi za migogoro na kutoelewana, na kusababisha hata vita kati ya mataifa
na ndani ya nchi. Na Maadhimisho yajayo yatakuwa ni ya kwanza kufanyika pamoja kiekumene.
Alieleza na kulezea tamko lililokwisha tolewa na Martin Junge, ambaye ni Katibu Mkuu
wa Shirikisho la Kilutheri Duniani, kwamba maadhimisho haya yatakuwa ya kimataifa,
hivyo ni vyema, kuwa ya kiekumene na ni wito kwa waamini wa makanisa kushuhudia
kimatendo umoja ulioombwa na Kristu mwenyewe.
Na kwamba , sababu ya mgawanyiko
wa Kanisa, mara nyingi tafasiri hukosewa na hivyo kwa mtazamo huo hata tafasiri
zake katika imani, teolojia na kidini. Kwa hiyo, katika mazungumzo ya kimataifa
ya kiekumeni, wamekuwa na uwezo wa kugundua upya misingi ya kawaida katika maswali
haya ya imani na waweza, kuwa na uwezo wa kueleza kwamba, hizi si sababu tena za
kuligawa Kanisa. ....
Na kwa upande wa Wakatoliki, imani juu ya mabadiliko
ndani ya Kanisa, yanakubalika kama ni ni jambo la kawaida katika safari yake 'Ecclesia
Semper reformanda' – ni kwamba maisha ya kanisa daima ni kutembea na marekebisho
wakati wote na katika kila umri, hivyo jambo la mageuzi linakuwa la kawaida pande
zote mbili, nini wameweza kufanya katika hati hii, ni kuonyesha mada kuu ya teolojia
ya Martin Luther kuwa yamekuwa ni maswala kwa ajii ya kanisa zima na vipengere muhimu
vya mageuzi katika Kanisa.