2013-06-18 15:05:54

Papa awaambia Waroma; Ninyi ni Mashahidi jasiri na wagonjwa


Jumatatu jioni, ukumbi wa Paulo V1 wa mjini Vatican, ulijaa nyuso za furaha na kicheko za mamia ya waamini kwa ajili ya Mkutano wa Kikanisa wa Jimbo la Roma uliofanyika chini ya Mada Kuu: Kristo muhimu: Jukumu la Wabatizwa kumtagaza Yesu Kristo.
Katika kufungua kazi za Mkutano huu, Papa Francisko, kabla ya kuingia ukumbini , pia alisalimia mamia ya waamini, waliobaki nje kufuatilia tukio hili nje kupitia Skrini kubwa ya Televisheni.
Ilani ya Katekesi ya Papa kwa ajili ya tukio hili , iliongozwa na Kauri mbiu:, Mimi sina aibu kuitangaza Injili, na alieleza juu ya dhamira ya sasa katika Uinjlishaji jimboni Roma na makandokando ambamo sasa kuna mabadiliko makubwa jamii ya kumezwa na hali za kidunia. Katika mkutano huu akiwepo pia Kardinali Agostino Vallini, Vika Mpya wa Jimbo la Roma.
Katekesi ya Papa, illiyojaa maisha sala, na tafakari zilizo lenga Ubatizo, Uinjilishaji na ujirani mwema kwa wakazi wa Roma, hasa maskini na watoto wadogo.
Mimi siionei aibu Injili ...Na kwenu wabatizwa hamko chini ya sheria bali chini ya neema. Papa ulitoa maneno haya ya Mtakatifu Paulo kwa Warumi, kama kielelelzo dhahiri katika katekesi yake, kueleza nini maana ya kuishi chini ya neema na uhusiano wake na uinjilishaliji. Neema ni furaha yetu, ni uhuru wetu kama wana wa Mungu ni mageuzi yaliyo badilisha moyo wa dhambi na katika utakatifu , kama Mtakatifu Paulo . Hii neema tuliyopewa bure lazima kuitoa, kwa moyo wa ukarimu na shukurani na uhuru kamili kwa wengine. . Hivyo ni rejea inaoelekeza katika hali halisi za raia wa Roma na wale wanaotafuta matumaini la kweli katika jamii na hawawezi kuipata huko.

Papa alieleza na kurejea hali zingine nyuma na za kuumiza zinazokabili wakazi wa Jimbo la Roma, ambamo alisema kuna wengi waliopoteza imani na wasiokuwa na matumaini. Hivyo alimtaka kila aliyekuwa akimsikiliza kufikiri kwa makini, na katika hali ya ukimya wa ndani ,juu ya watu hawa ambao wanaishi bila tumaini, wakiwa wamemezwa na huzuni kubwa na masononeko mengi ndani , wanaotoka kuzitoka hali hizo lakini wanatumia njia zisizoweza kuwatoa katika mahangaiko hayo, kama ulevi wa kupindukia katika unywaji wa pombe, dawa ya kulevya, kucheza kamari, fedha na ngono za fujo, mambo yasiyoweza kuwatoa katika shida zao.

Papa aliwahimiza waamini kwamba, ni i lazima kulionyesha tumaini na furaha ya Mkristu kwa watu hao. Lakini kwa namna gani? Ni rahisi, Papa alieleza, ni kupitia tabasamu na shuhuda msingi za ushindi wa Mkristu dhidi ya mambo ya kidunia. Lakini ushuhuda huu unahitaji ujasiri na uvumilivu, tabia mbili za Mtakatifu Paulo na Wakristo wote, na wale wanaotoka na kwenda kukutana na watu,waliotupwa pembezoni na hali za maisha.
Papa alikamilisha na kuialika jamii, kujenga ujasiri na uvumilivu, kwao wenyewe kwanza, ndipo watoke nje na kwenda huko ambako wanaume na wanawake wanaishi , kufanya kazi na kuteseka katka kuitangaza huruma ya Mungu, inayowafanya watu kumtambua Yesu Kristu wa Nazareti. Kutangaza Neema hii, tuliyopewa na Yesu .

Papa alieleza na kutahadharisha uwepo wa adui wengine, wanao wafanya waamini kuwa dhaifu katika uinjilishaji , akitaja kukata tamaa na woga, vinavyo shamirishwa na shetani ndani yetu: na hivyo kutengeneza vita vya kiroho, vyenye kuua Wakristu wengi, ambavyo ni lazima kuwa tayari, kupambana.
Hakuna sababu za kuogopa kwa sababi silaha katika mapambano haya ni upendo, upendo wa Mungu, Baba yetu. Usiogope kupokea neema ya Yesu Kristo, wala kuwa na hofu juu ya uhuru wako, kwa kuwa uhuru huo unatoka katika neema ya Yesu Kristo, au, kama Paulo alisema, "wewe si chini ya Sheria bali chini ya neema. Papa alihoji wake kwa waume waliokwisha ipokea neema hiyo wakati wa Ubatizo, inakuwaje wanaogopa kuitangaza? Ni neema ambayo Yesu anawapa waamini , neema isiyo gharamu kitu, bali kuipokea na kuitunza.








All the contents on this site are copyrighted ©.