2013-06-18 10:33:46

Makanisa manne yachomwa moto nchini Nigeria


Kikundi cha Boko Haram kimechoma Makanisa manne, kikapora mifugo na chakula, kiasi cha kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi wa maeneo yaliyoko Kaskazini mwa Nigeria.

Askofu mkuu Ignatius Ayau Kaigama, Rais wa Baraza la Maskofu Katoliki Nigeria anasema, kwamba, hadi sasa hakuna taarifa zaidi kutokana na sehemu hizi kukatiwa mawasiliano kama sehemu ya mchakato wa oporesheni maalum ya kupambana na Kikundi cha Kigaidi cha Boko Haram, Kaskazini mwa Nigeria.

Kutokana na operesheni maalum iliyoanzishwa na Serikali kwa kutangaza hali ya hatari, wananchi kwa kiasi fulani wanajisikia kuwa na usalama, ingawa bado Kikundi cha Boko Haram kinaendelea kushirikiana na Kikundi cha Jihadi kilichosmbaratishwa kutoka nchini Mali.

Baraza la Maaskofu Nigeria linasema, wananchi wa Nigeria kwa sasa wanalipa gharama kubwa ya uzembe ambao ulisababishwa na vikosi vya ulinzi na usalama kushindwa kudhibiti Kikosi cha Boko Haram tangu mwanzo. Kwa sasa kuna haja ya kushirikiana kati ya Nigeria, Niger na Mali ili kuondokana na vikundi hivi vinavyoendelea kutishia usalama wa maisha ya raia na mali zao anasema Askofu mkuu Kaigama.







All the contents on this site are copyrighted ©.