2013-06-18 10:05:54

Bwana Ken hackett ateuliwa kuwa Balozi wa Marekani mjini Vatican


Rais Barack Obama wa Marekani amemteua Bwana Ken Hackett, kuwa Balozi wa Marekani mjini Vatican. Bwana Hackett kwa takribani miaka 40 amekuwa akifanya kazi na Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki nchini Marekani hadi mwaka 2012. Amewahi pia kufanya kazi zake Afrika Mashariki, Sierra Leone na pia kama Balozi wa Marekani nchini Ufilippini kuanzia mwaka 1987 hadi mwaka 1992.

Kuanzia mwaka 1996 hadi mwaka 2004 alikuwa ni Makamu wa Rais Caritas Internationalis nchini Marekani. Kati ya mwaka 1996 hadi mwaka 2011 alikuwa ni mjumbe wa Cor Unum. Na mwaka 2004 hadi mwaka 2009 alikuwa ni Mkurugenzi wa bodi ya wakurugenzi wa MCC. Uteuzi huu unasubiri kuthibitishwa na Congress ya Marekani.







All the contents on this site are copyrighted ©.