2013-06-17 16:03:38

Urafiki na maridhiano kati ya dini ni sharti msingi katika ujenzi wa amani.


Ziara ya Kardinali Jean Louis, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Majadiliano na dini zingine, akirejea ziara yake ya wiki iliyopita nchini Uingereza, ameitaja kuwa ya mafanikio, imekuwa ni ya kujielemisha zaidi na pia kuwa msaada chanya katika ujenzi wa mahusiano imara zaidi kati ya waamini wa dini zingine mbalimbali.
Kardinali Jean-Louis Tauran, mapema siku ya Ijumaa, aliongoza Ibada ya Misa katika Kanisa Kuu la Westminster , Misa iliyo hitimisha ziara yake ya siku tano , aliyoifanya kwa lengo la kuimarisha majadiliano kati ya dini mbalimbali na ujenzi wa mahusiano mema baina ya dini na dini, na kuonyesha kwamba, urafiki kati ya dini ni sharti msingi katika ujenzi wa amani na maridhiano. .
Siku hiyo, Kardinali Tauran, pia alikutana na jumuiya Wahindu, Wajain na Kalasinga, katika ukumbi wa Kanisa Kuu la Westminster, kabla ya kuadhimisha Ibada ya Misa, akisaidiana na , Askofu Mkuu Vincent Nichols wa Westminster.
Katika homilia yake wakati wa Ibada , Kardinali Tauran alisema, katika dunia inayozidi kuwa na dini mbalimbali, linakuwa ni jambo la lazima kuishi kwa umoja na upendo na watu wa tamaduni nyingine za kidini, hali iliyogeuka kuwa halisi na isiyo weza kuepukika, na hivyo Kanisa linawahimiza wamumini wake kama anavyosema Papa Francis, kujenga madaraja kati ya watu wote, ili kwamba kila mtu aweze kumfikia mwingine si kama adui, au mshindani, lakini kama ndugu. kumpokea na kumkubatia kwa jinsi alivyo.
Katika mtazamo huo, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Majadiliano ya Kidini, aliwahimza wote waliokuwa wakimsikilzia kuanzisha uhusiano mzuri na majirani wao, na waamini wa dini nyingine, kama silaha ya kukuza amani. Aliendelea kutoa maneno ya Pius XII, ambaye mwaka 1946 alisema "dhambi ya karne hii ni watu kupotelea katika dhambi. Kardinali alionyesha jinsi, kupita kwa miaka sitini saba baadaye, bado dunia inazidi kulemewa na ukana Mungu unao ongeza migororo nyenye kubomoa imani na kuleta mtafaruko wa kidini kati ya waumini.
Kardinali Tauran, alihitimisha hotuba yake kwa kurudia onyo lililotolewa na Papa Francis Papa , wakati wa Jumapili ya Pasaka mwaka huu, kwamba, tunatakiwa kuwa vyombo ya huruma ya Mungu, kupitia njia ambazo Mungu atazifanikisha hapa duniani, na kwa ajili ya utetezi wa viumbe wote na kushamirisha haki na amani.










All the contents on this site are copyrighted ©.