2013-06-17 08:55:02

Papa asema ;fedha, siasa na uchumi ni kwa ajili ya kuhudumia watu na si mamlaka


Baba Mtakatifu Francis ameaasa kwamba, fedha, siasa na uchumi ni kwa ajili ya kuhudumia watu na si mamlaka. Ni lazima kuwatumikia watu hasa katika kukuza maadili ya ukweli katika jamii. Huo ni ujumbe wa Papa, kwa Waziri Mkuu wa Uingereza, juu ya kikao kijacho cha Baraza la G8.
Papa ametoa ujumbe huo kupitia barua aliyomtumia Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron, kama jibu kwa barua ya Waziri Mkuu Cameron kwa Papa, iliyolenga katika uwepo wa kikao cha G8 huko Ireland Kaskazini. Kikao kinachokusanya viongozi wa mataifa yenye uwezo zaidi wa kifedha duniani.
Katika barua yake, Papa Francis amesifu vipaumbele vya ajenda zilzotolewa na Uenyekeiti wa G8 yaani soko hurua la Kimataifa, kodi, na uwazi kwa upande wa serikali na watendaji wa kiuchumi; utendaji thabiti wa pamoja kwa ajili ya kufuta njaa na uwepo wa uhakika wa chakula na utetezi wa makundi dhaifu katika jamii, wanawake na watoto dhidi ya ukatili wa kinjisia hasa wakati wa machafuko ya kisiasa na hali za kivita.
Katika mtazamo huo, Papa, ameandika kwamba G8 "haweizi kushindwa kushughulikia hali za machafuko kama yale yanayoendelea Mashariki ya Kati, hasa katika Syria. Ameonyesha tumaini lake kwamba, Kikao hicho cha G 8, kitasaidia kupata "kwa haraka tena kwa kudumu jibu la kusitisha mapigano na kuvileta pamoja katika meza ya majadiliano vyama vyote husika nchini Syria, kuzungumzia amani . Amani ni jambo muhimu katika ufanikishaji wa juhudi zote zinazolenga kulinda na kutetea watu wahitaji kama wanawake na watoto na wazee na kafara wote wasiokuwa na hatia ambao wa sasa wanaathirika kwa njaa .

Papa Francis ameandika kwamba, katika muonekano wa kweli kinzani, uhuru na mshikamano , ni muhimu katika utendaji laini wa uchumi wa dunia.

Na kwa namna hiyo anamalizia barua yake, kila mfumo wa kiuchumi na nadharia za kisasa au utendaji, ni lazima ulenge katika kutoa kwa kila mkazi wa dunia hii, mahali popopte alipo, kuishi kwa hadhi na uhuru, pamoja na uwezekano wa kukidhi mahitaji ya familia, elimu kwa watoto, ibada kwa Mungu, na fursa ya kuedeleza uwezo wake mwenyewe. Hili ni jambo kuu muhimu , na bila ya mtazamo huo , shughuli zote za kiuchumi hazina maana.










All the contents on this site are copyrighted ©.