2013-06-17 09:29:19

Mkutano wa G8 na changamoto zake!


Uchumi wa kimataifa, mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa; ulinzi na usalama ni kati ya mambo makuu yanayojadiliwa na Wakuu wa G8 wanaoanza mkutano wao mkuu wa mwaka kuanzia tarehe 17 hadi 18 Juni 2013 huko Ireland ya Kaskazini. Syria, Afghanstan na Bara la Afrika ni kati ya masuala tete yanayojadiliwa na viongozi hawa pamoja na Wawakilishi kutoka Barani Afrika.

Wakuu wa G8 wanajadili pia mbinu mkakati utakaoziwezesha nchi zao kuvuka kikwazo cha athari za myumbo wa uchumi kimataifa ambao umepelekea ukosefu wa ajira kwa vijana wengi duniani pamoja na kuendelea kufanya mabadiliko makubwa katika Shirika la Fedha Kimataifa.







All the contents on this site are copyrighted ©.