2013-06-17 16:14:51

Kutetea maisha ya binadamu si tu haki na wajibu kwa Wakristu, lakini ni wajibu kwa watu wote, Askofu Mkuu Fischella.


Jumapili wakati wa kukamilisha Ibada ya Misa katika Kanisa Kuu la Mtaktifu Petro, Askofu Mkuu Rino Fischella, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Kukuza Uinjilishaji Mpya , alitoa salam zake kwa Baba Mtakatifu Fransisko, kwa ajili ya adhimisho hili la Siku ya Injili ya Maisha. .
Katika salaam hizo , kwanza aliutambulisha Umati wa waaamini waliohudhuria Ibada ya Misa akisema, wingi wa watu hawa waliotoka pande mbalimbali za duniani , ni ushuhuda dhahiri kama Injili ya Yohana inavyosema, maisha yamedhihirishwa.
Katika salaam hizi, Askofu Mkuu Fisichella, alionyesha shukurani za dhati kwa Papa kwa msaada wake na nguvu za ushahidi wake, katika kuyatetea na kuyalinda maisha.
Katika maadhimisho ya Ibada ya Misa siku ya Jumamosi asubuhi, umati mkubwa wa wawakilishi wa vyombo vya kutetea maisha , wake kwa waume walihudhuria ibada hiyo kwa ajili ya maadhiisho Siku ya Injili ya Maisha, ikiwa ni alama ya neema kuguuguswa na mwili wa Kristo na hivyo kuwa watetezi imara wa hadhi ya maisha.
Askofu Mkuu Fischella, aliutaja umati huo, kuwa ni mashahidi wa upendo, ambao kamwe haukosi kuwa karibu na watoto na walio telekezwa, wenye kusumbuliwa na maradhi sugu, walemavu, watu walio katika hali za kufa na waliotupwa pembezoni na jamii, kwa tamaa za dhambi na ubinafsi wa mtu.
Na aliogeza katika Mwaka wa Imani, inakuwa ni wakati muhimu wa kutafakati na kusali kwa ajili ya wale wanao yatolea maisha yao kama mashahidi wa Injili ya Maisha. Shauku ya maisha yao ya kila siku inaonyesha wazi dhamira ya kukuza kikamilifu zawadi ya maisha ya binadamu na kwa ajili ya utetezi wake. Kufanywa upya katika wito kwa kila mtu na kuheshimu, kulinda, kupenda na kumtumikia maisha ya binadamu, si tu haki na wajibu wa Wakristo, lakini ni maisha ya kawaida kwa watu wote , wanaume kwa wanawake, hata ambao si Wakristu.







All the contents on this site are copyrighted ©.