2013-06-15 14:23:57

Mheshimiwa Padre Xavier Munyongani ateuliwa kuwa Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Gweru, Zimbabwe


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Xavier Munyongani wa Jimbo Katoliki la Masvingo, Padre mshauri wa maisha ya kiroho wa Jumuiya ya Waamini wa Kanisa Katoliki kutoka Zimbabwe wanaoishi nchini Uingereza kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Gweru, nchini Zimbabwe.

Askofu mteule alizaliwa tarehe Mosi, Januari 1950 Jimboni Masvingo. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapadrishwa kunako tarehe 20 Agosti 1977 kwa ajili ya Jimbo Katoliki Gweru na baadaye, akajikuta akiwa kwenye Jimbo la Masvingo lililoundwa kunako mwaka 1999.

Jimbo Katoliki la Gweru lilianzishwa kunako mwaka 1955 ni sehemu ya Jimbo kuu la Bulawayo, Zimbabwe. Jimbo lilikuwa wazi kuanzia mwezi Aprili 2012 baada ya Askofu Martin Munyanyi kung'atuka kutoka madarakani.







All the contents on this site are copyrighted ©.