2013-06-14 09:02:06

Mtumishi wa Mungu Odoardo Focherini kutangazwa kuwa Mwenyeheri


Mama Kanisa tarehe 15 Juni 2013 anatarajia kumtangaza Mtumishi wa Mungu Odoardo Focherini kuwa Mwenyeheri. Huyu ni mwamini mlei, baba wa watoto saba, mwandishi wa habari na mkurugenzi wa Gazeti la “L’Avvenire di Italia” huko Capri, Kusini mwa Italia. Oduardo Focherini aliuwawa kikatili kutokana na chuki za kiimani. 00:00:50:50

Ni mwamini mlei aliyejitoa kimaso maso kwa ajili ya kuwalinda na kuwaokoa Wayahudi zaidi ya 100 waliokuwa wako hatarini kupelekwa uhamishoni. Kitendo hiki kilihatarisha maisha yake, kiasi kwamba, akakamatwa na kutiwa gerezani kutokana na chuki dhidi ya Imani ya Kanisa Katoliki.

Kutokana na mateso na madhulumu makali, kunako mwaka 1944 akaitupa mkono dunia, akiwa kijana mwenye umri wa miaka 37. Ni mwamini wa kwanza kutoka Italia kutangazwa na Mama Kanisa kwa kusimama kidete kulinda na kutetea maisha ya Wayahudi dhidi ya dhuluma na nyanyaso za utawala wa Kinaz







All the contents on this site are copyrighted ©.