Mh. Padre Luiz Fernando Lisboa ateuliwa na Papa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Pemba,
Msumbiji
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Luiz Fernando Lisboa kuwa Askofu
wa Jimbo Katoliki Pemba, nchini Msumbiji. Askofu mteule alizaliwa tarehe 23 Desemba
1955 mjini Rio de Janeiro, Brazil. Baada ya majiundo yake ya kitawa kwenye Shirika
la Mapadre wa Mateso, tarehe 23 Januari 1977 aliweka nadhiri zake za mwanzo na tarehe
18 Desemba 1982 akaweka nadhiri za daima.
Baada ya masomo na majiundo yake
ya kikasisi, akapadrishwa tarehe 10 Desemba 1983. Katika maisha na utume wake kama
Padre na mtawa amejishughulisha zaidi na masuala ya kichungaji Parokiani; malezi seminarini.
Kuanzia mwaka 2001 hadi mwaka 2010 alitekeleza utume wake kama Paroko, Jimbo Katoliki
la Pemba, Msumbiji na mkufunzi wa masuala ya kitaalimungu kwa waamini walei. Baadaye
alirejea nchini Brazil kwa mapumziko mafupi.